Sunday, July 27, 2008

HICHI NDIO KIZAZI KIPYA CHA MTANZANIA HALISI



Picha ni wadogo/watoto wetu katika majira mawili tofauti jua na mvua sasa kweli jamii yetu itegemee kizazi cha aina gani hapo mbeleni kutoka kwa watoto hawa..

Hivi hasa tatizo liko kwa Serikali ama mwananchi/raia ambaye amaamua kuwa nawatoto bila mipangilio kwa imani kila mmoja atakuja na Baraka/riziki zake nini hasa kifanyike WAZUIWE WATU KUWA NA WATOTO LUKUKIKI KAMA WENZETU WA CHINA?maaana haiana maana kuwa na watoto bora watoto..

Thursday, July 24, 2008

UZALENDO WAWASHINDA SHOPRITE



Wafanyakazi wa Shoprite (KAMATA)leo asubuhi wameshikamana kumtetea Mfanyakazi wenzao dhidi ya maamuzi ya kinevu ya Uongozi,Huku wakiimba nyimbo kuonyesha mshikamano na wengine wakiwa wamebeba mabango yenye Ujumbe.."UBADHIRIFU UNAOFANYWA NA KAMPUNI UNAMGHARIMU MFANYAKAZI WA KAWAIDA ASIYE NA HATIA MWAJIRI ARUDI KWENYWE MEZA YA MAJADILIANO"
Haikufahamika mara moja ni kitu gani kilichopelekea kufikia hatua hiyo,Kwa siku za usono kumekuwa na malalamiko kuhusiana na utendaji mzima wa Shoprite hasa kuhusiswa na Vitendo vya WIZI.

Wednesday, July 23, 2008

KIBAKA ACHOMWA MOTO LEO ASUBUHI




Kachomwa mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa..

Mwanaume mmoja kachomwa moto leo asubuhi majira saa moja 7:00 kwa kusadikiwa kuwa ni kibaka eneo la Ilala boma mbele ya ofisi ya Mkuu wa mkoa
Suala la Watanganyika kujichukulia Sheria mikonono kwa watuhumiwa wa Ukibaka limekuwa la kawaida sasa kwa maisha magumu ya kila siku..
Sijui tumlaumu nani... Kibaka aliyeiba/kwapua au..Mtanganyika aliyejichukulia Sheria

Thursday, July 17, 2008

UPANUZI WA BANDARI YETU YA DAR ES SALAAM



Kama inavyoonekana ubomoaji wa nyumba kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka Bandari umekuwa wa kusuasua japokuwa tarehe ya mwisho ya kuvunja nyumbazao kwa hiyari ikiwa tayari ishapita SIJUI UPANUZI WA BANDARI UTAANZA LINI....

Thursday, July 3, 2008

HAYA NDIO MAISHA YA KILA SIKU MARA CONTAINERS MARA MAGOROFA BORA SIKU ZIENDE..





NDUGU ZANGU HAYA SASA TUMESHAYAZOEA KILA KITU KINACHUKUA NAFASI YAKE,USISHANGAE KUSKIA NA WATU NAO WANAANZA KUANGUKA KWA NJAA... KAMA UNAVYOONA HAPO GARI LIKIDONDOSHA CONTAINER HII YOTE MAMLAKA ZINAZOHUSIKA KUTOKUTEKELEZA WAJIBU

Wednesday, July 2, 2008

BONGO KILA MTU MBABE.....



JANA WAKATI NARUDI USWAZI MAENEO YA KIGOGO UKIANZA TU KUSHUKA KALE KAMLIMA NIPO KWENYE FOLENI FLAN YA KIZUSHI JAMAA WALA SIJUIA ALIKOTOKEA KAJA KANICHOMEKEA KWA MBELE DUH. NIKAWAHI KUFUNGA BREAK BILA HIVYO INGEKUWA BALAA ILA SHWARI TUKAMALIZANA KIBONGO ILA ROMEO KAUMIA KIMTINDO..